Sujuda kwako Mwalimu

Na Issa Bin Mariam

Nikaona kwa macho yangu
nikasikia kwa masikio yangu
mwalimu akikimbia
kuwahi shuleni

tip-tap, tip-tap, tip-tap
viatu vya kike vinalalamika
mwendo ule ule, lengo lilelile
kuwahi shuleni

mwalimu kanusa
mwalimu kaona
vijana wake wawili
wanacheza miferejini

kawagombeza
kawa amrisha
“tokeni, tokeni”
kaendelea, kuwahi shuleni

heshima zangu kwako mwalimu
sujuda zangu kwako mwalimu
uuishi milele
ualimu wako mwalimu

anakusihi mwalimu mwenzako
popote endako
utunze heshima zako
ni tuzo lako, kutoka jamii yako

unachofanya mwalimu
unatushinda sisi wazazi
unajenga binadamu
mwenye utu na ubinadamu

Advertisements
Categories:

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s